Song of Solomon 1

1 aWimbo ulio bora wa Sulemani.

Shairi La Kwanza

Mpendwa


2 bUnibusu kwa busu la kinywa chako,
kwa maana upendo wako unafurahisha kuliko divai.

3 cManukato yako yananukia vizuri,
jina lako ni kama manukato yaliyomiminwa.
Ndiyo sababu wanawali wanakupenda!

4 dNichukue twende nawe, na tufanye haraka!
Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake.

Marafiki

Tunakushangilia na kukufurahia,
tutasifu upendo wako zaidi kuliko divai.

Mpendwa

Tazama jinsi ilivyo bora wakupende!

5 eMimi ni mweusi, lakini napendeza,
enyi binti za Yerusalemu,
mweusi kama mahema ya Kedari,
kama mapazia ya hema la Sulemani.

6 fUsinikazie macho kwa sababu mimi ni mweusi,
kwa sababu nimefanywa mweusi na jua.
Wana wa mama yangu walinikasirikia
na kunifanya niwe mtunza mashamba ya mizabibu.
Shamba langu mwenyewe la mizabibu nimeliacha.

7 gNiambie, wewe ambaye ninakupenda,
unalisha wapi kundi lako la kondoo
na ni wapi unapowapumzisha kondoo wako adhuhuri.
Kwa nini niwe kama mwanamke aliyefunikwa shela
karibu na makundi ya rafiki zako?

Marafiki


8 hKama hujui, ewe mwanamke mzuri kuliko wote,
fuata nyayo za kondoo,
na kulisha wana-mbuzi wako
karibu na hema za wachungaji.

Mpenzi


9 iMpenzi wangu, ninakufananisha na farasi jike
aliyefungwa katika mojawapo ya magari ya vita ya Farao.

10 jMashavu yako yanapendeza yakiwa na vipuli,
shingo yako ikiwa na mikufu ya vito.

11 Tutakufanyia vipuli vya dhahabu,
vyenye kupambwa kwa fedha.

Mpendwa


12 kWakati mfalme alipokuwa mezani pake,
manukato yangu yalisambaza harufu yake nzuri.

13 lMpenzi wangu kwangu mimi ni kifuko cha manemane
kati ya matiti yangu.

14 m nMpenzi wangu kwangu mimi ni kama kishada cha maua ya mhina
kutoka mashamba ya mizabibu ya En-Gedi.

Mpenzi


15 oTazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu!
Tazama jinsi ulivyo mzuri!
Macho yako ni kama ya hua.

Mpendwa


16 Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu!
Ee, tazama jinsi unavyopendeza!
Na kitanda chetu ni cha majani mazuri.

Mpenzi


17 pNguzo za nyumba yetu ni mierezi,
na mapao yetu ni miberoshi.
Copyright information for SwhKC